Breaking

Dalili za awali za mimba kuharibika

Image result for mimba kuharibika
Leo tumeamua kuzungumzia jambo hili ambalo huwakumba watu wengi sana katika familia zao, wengi wamekuwa wakitokewa na jambo hili katika mimba zao za kwanza na mimba zao zinazoendelea katika familia zao na kushindwa kupata watoto.

Kuna wengine wanapata watoto au mtoto mmoja na baadaye wanashindwa kupata mtoto kwa sababu ya mimba zao kuwa zinaharibika mara kwa mara.

Kwa kawaida kitabibu inaaminika kwamba asilimia 50 ya mimba zote huwa zinaharibika, najua watu wengi wanaweza wakashangaa lakini ni kweli tafiti za kitabibu zinasema hivyo isipokuwa watu wengi huwa hawaelewi au wanawake wengi huwa hawaelewi kama mimba zao zimeharibika kwani hutoka au huaribika kabla wao hawajagundua kama walikuwa wajawazito.

Isipokuwa wale ambao hujua kwamba walikuwa na ujauzito na umetoka hao wanaweza kuwa asilimia 10 hadi 20, na hizo asilimia zinazobaki kama 35 ni kwa wale ambao hawajui kama mimba zao zimeharibika au walikuwa wajawazito.

Kwa maana hiyo basi wewe ambaye unatafuta ujauzito kwa muda mrefu sasa na umekuwa haupati lakini unakuwa unaandamwa na matatizo ya hedhi kwa mara kadhaa halafu hedhi inakaa sawa basi kuna uwezekano mkubwa kwamba mimba zako zimekuwa zikiharibika pasipo wewe kujua.

Dalili za kuharibika kwa mimba 
Ni vizuri kujua ni dalili zipi ambazo mtu akiziona basi kunakuwa na uwezekano wa kuharibika kwa mimba, kwani mimba huweza kuharibika hadi wiki ya 20 (miezi 5) kuanzia siku ya kwanza inapoingia, japo hasahasa hutokea katika miezi mitatu ya mwanzo (1st trimester) lakini huweza fika hadi wiki ya 20.

Na dalili hizo ni kama;

Damu nyepesi kutoka kwa mwanamke mwenye mimba.
pale mwanamke anapopata ujauzito basi ni vema kabisa kujua kwamba hatakiwi kabisa kupata hedhi au kutokwa na damu katika via vyake vya uzazi, kwa maana hiyo basi wewe mwanamke ambaye umepata ujauzito na bado unaona damu inatoka kidogokidogo basi ni vema kuwahi mapema kituo cha afya kabla tatizo halijawa kubwa kwani kutoka kwa mimba (miscarriage) huwa hakutokei ghafla tu huanza taratibu na dalili yake kubwa ni hii kutokwa na damu ilihali wewe ni mjamzito.

kutokwa na damu yenye mabonge mabonge na inakuwa nzito 
Wakati mwingine  mwanamke anaweza akakumbwa na kutokwa na damu nyepesi na kabla hajatahamaki, damu ile nzito inaanza kutoka tena, na hii ni dalili mbaya sana ya kwamba ujauzito wako uko kwenye hatari zaidi na kuna uwezekano ujauzito ulionao ukatoka, kwa maana hiyo basi mwanamke anapopatwa na dalili ile ya kwanza ni vema zaidi kufuata ushauri wa daktari ili kuulinda ujauzito wako.

Uchovu na maumivu makali ya kiuno na mgongo.
kwa wewe mwanamke ambaye mimba bado ni changa na unapatwa na maumivu makali sana ya mgongo au kiuno au vyote kwa pamoja basi ni vema kuwahi kituo cha afya ili kuangalia ni jinsi gani unaweza kuzuia ujauzito wako usitoke au usikumbwe na tatizo hili la kutokwa na ujauzito (miscarriage).

Kama unapatwa na dalili kama hizi kutokwa na damu nyepesi au nzito ilihali wewe ni mjamzito basi ni vema kuwahi kituo cha afya au wasiliana nasi ili kukusaidia. Kwa ushauri vipimo na tiba dokta anapatikana kwenye vituo vyake vya Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Mwanza.

Maoni 2 :

  1. Enter your comment...ninampenzi wangu tumekutana nae sku za hatari lakini leo anadai anatoka damu sehemu za siri na damu izo zipo mixer nyepez na nzito tatizo ni nini nisaidid

    JibuFuta
    Majibu
    1. Asante ndugu peter kwa kutembekea blog yangu.. Naanza kukujib swali lako kama ifuatavyo.

      Hali ya tendo la ndoa inaweza kusababisha uke kuchubuka. Hali hii inaweza kusababisha kutokwa na damu ambayo huchanganyakana na uchafu wako na kuwa wa kahawia au wenye damu.
      Baada ya tendo la ndoa katika siku za hatari, huwa kuna nafasi kubwa mno ya kupata ujauzito. Ikiwa kama mbegu zitarutubisha yai, basi ndipo kiinite hutengenezwa. Kiinitete hubebwa na kusafirishwa kwenda kwenye kifuko cha uzazi(uterus) ambapo hupandikizwa ama kupachikwa kwenye ukuta wa mfumko wa kizazi(uterus) ambao kitaalamu hujulikana kama endometrium.kiinitete hicho husabsbisha mgandamizo wa damu

      Endapo kama hali hii ya mgandamizo itatokea, basi huwa kuna kunatokea hali ya kutokwa na damu kidogo kutoka kwenye ukuta wa mfuko wa kizazi(endometrium) ambayo huchangamana na utoko au uchafu na kuwa kama damu yenye utelezi kama makamasi vile.
      damu yenye utelezi inapojitokeza hukoma ndani ya masaa au siku chache tu. Ikiwa kama utaona damu nyeusi inatoka baada ya kufanya tendo la ndoa, basi itakuwa ni dalili za uvimbe kwenye mfuko wa kizazi(uterus) kama vile Fibroids. Kwa hali hii usichelewe kabisa. Yafaa sasa ufike hospitali ili kufanya uchunguzi wa vipimo.

      Futa

Inaendeshwa na Blogger.