Breaking

"Nipo tayari kushirikiana na serikali

Image result for nandy

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Nandy amefunguka na kuweka wazi kuwa kitendo cha video yake ya faragha akiwa na msanii mwenzake Bill Nas kuvuja kimempa somo kuwa siyo sahihi kujichukua video za utupu na kusambaa kwenye mitandao.

Nandy ameweka wazi hayo jana April 19, 2018 baada ya kutoka katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kusema amejutia sana jambo hilo na kudai sasa yupo tayari kushirikiana na serikali kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi na watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifanya hivyo bila kujijua kuwa wanafanya makosa.

"Nipo tayari kushirikiana na serikali kwa hili lililotokea kuelimisha wasanii, wanafunzi na jamii kiujumla najua watu wengi wanapitia hatua kama hizi na wengine hata hawajulikani lakini kwa kuwa limetokea kwangu ila najua kuna wengine wamefanya mambo kama haya na video zimekwenda kwenye mitandao hata bila idhini yao" alisema Nandy

Mbali na hilo Nandy amesema kuwa suala la mtu ambaye amesambaza video zake hizo bado lipo polisi na kuwa anaamini kuwa jeshi la polisi litakuja na majibu mazuri kuhusu suala hilo lakini pia amewaombea radhi watu ambao wamefanya jambo hilo.

"Naomba radhi kwa niaba ya watu ambao wamefanya kitendo cha kusambaza video hiyo japo nashukuru jeshi la polisi linaendelea kupambania naamini watakuja na majibu mazuri, pia naomba radhi kwa mashabiki kwa kuweza kuona video hiyo kwani haikuwa makusudio yangu kabisa kitu hicho kitokee" alisisitiza Nandy.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.