Breaking

Utata Nafasi ya Lionel Mess, Coutinho

Image result for messi
Kocha wa Barcelona Ernesto Valverde ameeleza kuwa majukumu ya wacheaji wake nyota Lionel Messi na mchezaji ghali zaidi wa klabu hiyo Philippe Coutinho yanabadilika kutokana na aina ya mchezo.


Akiongea baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Valencia jana usiku, Valverde alisema Coutinho analazimika kucheza kiungo cha katikakati kutokana na Messi kupenda kucheza winga ya kulia lakini muda mwingine anaingia katikati kusaidia timu.

"Ni kweli Coutinho namchezesha katikati kwa sababu wakati mwingine Messi anapenda kucheza upande wa kulia, lakini tayari nimeshajua namna ya kumtumia badala ya kucheza kulia atakuwa anacheza pande zote mbili ili kumpa nafasi Messi upande wa kulia pamoja na katikati'', amesema.

Valverde ametetea pia uamzi wake wa kumchezesha Coutinho upande wa kulia ni kwasababu mchezasji huyo hucheza vizuri kwenye eneo hilo akiwa na Brazil ambayo inacheza soka sawa na Barcelona lakini ameona ampe nafasi kucheza winga zote huku akimwacha Messi acheze kila mahali.

Aidha kocha huyo raia wa Hispania pia amesema wanahitaji kumpumzisha Messi na majukumu makubwa ndani ya klabu. Messi jana alisaidia kupatikana kwa bao hilo moja baada ya krosi yake kuunganishwa kwa kichwa na Luis Suarez. 

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.