Breaking

Faida za kula nanasi kiafya

Image result for nanasi
Nanasi lina vitamin A, B, C lakini pia lina madini ya chuma, calcium, phosphorus na copper. Pindi mtu atumiapo tunda hili  lina uwezo mkubwa wa kuimarisha  mifupa, meno. Misuli na neva za mwili.

Ingawa wapo baadhi ya watu huwa hawapendi kutumia tunda hilin eti kwa madani ya kwamba huwa linawasha kwenye ngozi yam domo mara baada ya kulitumia, inawezekana watu hao wakawa sawa ila ukweli ni kwamba achana na kuwasha kwa mdomo bali wewe angalia faida zitakonazo na tunda hilo.

Zifaatazo ni faida za kula tunda hilo;

1.    Husaidia kwa kiwango kikubwa kwa wale wenye matatizo ya choo.

2.    Lakini pia inashauriwa ya kwamba kwa wakina mama wajawazito na wale wanyonyeshao walitumie nanasi kwa wingi kwa sababu  lina faida lukuki sana.

3.    Kwa wale wenye matitizo ya athma pia wanashauriwa walitumie tunda hili kwani lina uwezo wa kutibu ugonjwa huo.

4.    Lakini pia miongoni mwa matunda ambayo yana uwezo wa kurudisha kumbukumbu ni tunda hili, hivyo basi kwa wale ambao wana matatizo haya  ya kupoteza kumbukumbu wanashauriwa kutumia tunda hili.

5.    Lakini pia kwa wale wenye matatizo ya utumbo mwembamba na magonjwa ya koo wanashauriwa watumie tunda hili kwani husaidia sana kutibu magonjwa hayo.


Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.