Mourinho ajashangazwa na kiwango cha sanchez
Baada ya nyota mpya wa Manchester United Alexis Sanchez kucheza mechi yake ya kwanza kwenye klabu hiyo kocha Jose Mourinho amesema hajashangazwa na kiwango cha nyota huyo.
Mourinho ambaye amesaini mkataba mpya juzi wa kuendelea kuinoa klabu hiyo, amesema kiwango cha Sanchez hakijamshangaza kwani ni mchezaji wa daraja la juu hivyo kuonesha makali katika mechi yake ya kwanza ni kitu ambacho alikitegemea.
Sanchez alianzishwa jana kwenye kikosi cha kwanza cha United ambayo amejiunga nayo hivi karibuni akitokea Arsenal na kuisaidia kushinda 4-0 dhidi ya wenyeji Yeovil Town katika mechi ya raundi ya nne Kombe la FA.
Sanchez mwenye umri wa miaka 29, huenda akaendelea kuaminiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza kitakacho kabiliana na Tottenham Hospurs kwenye mchezo wa EPL Jumatatno ijayo.
Hakuna maoni: