Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu.
Si kila ufanyiwacho ni lazima umwambie kila mtu.
Ipo nguvu katika kunyamaza
Yapo mambo ambayo tunapaswa kuongea, kusema, lakini yapo mambo ambayo tunapaswa kunyamaza kwa ajili ya usalama wa Roho zetu.
Ni kweli kuna wakati unasemwa sana vibaya, unasingiziwa, unatukanwa nk nk, lakini ni lazima ukumbuke kwamba kuna mazingira ambayo hupaswi kujibizana hata kama umeumia kiasi gani.
Unajua ni kwanini?
Ukisemwa vibaya, ukitukanwa, ukidharauliwa lazima moyo utaghafilika, moyo ukighafilika lazima utakuwa na hasira na ghadhabu.
Ukiwa na hasira katu usitegemee kuwa utajadiliana na mtu kwa hekima.
Ukiongea utaongea katika uwepo wa hasira, ukijibu utajibu kulingana na kiwango cha hasira ulichonacho.
Sasa jiulize majibu yanayotoka kutokana na msukumo wa hasira huwa yanakuwaje?* Mazuri? Ya upole? Ya hekima? Ya unyenyekevu? I am sure jibu ni hapana.
Kama jibu ni hapana that means utaongea vitu vibaya ambavyo ni chukizo kwa MUNGU kwa sababu amesema maneno yetu na yakolee munyu (chumvi). Ni vyema sisi pia tukajifunza kusoma mazingira na nyakati na hali za watu zilivyo ili tujue ni wakati gani tujibu, tuongee nini na ni wakati gani tunyamaze
Kilinde kinywa, hakikisha haukiachi kinene mabaya
Usipoteze marafiki na kuharibu mahusiano kwa ajili ya kinywa kibovu
Ni kweli moyo na akili na hisia vinakusukuma kujibu, kubisha nk nk, lakini elewa impact za kujibizana ukiwa na hasira na hizo ni bora ukae kimya.
AKUSHINDAE KUONGEA, MSHINDE KWA KUNYAMAZA
Hakuna maoni: