Mourinho aongezewa muda United
Akiwa amebakiza mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika kocha wa Manchester United Jose Mourinho ameaminiwa kuendelea kuifundisha timu hiyo hadi mwaka 2020.
Baada ya jana usiku kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kocha Jose Mourinho amesema anafuraha kuona timu kubwa yenye historia kubwa duniani kama United imeendelea kuamini kwamba yeye ni kocha sahihi kwa timu hiyo.
''Najisikia mwenye thamani kupewa fursa ya kuendelea kuongoza kundi la vijana wenye ubora na uwezo mkubwa katika soka hivyo naamini tutafikia malengo ya timu'', ameongeza
Mourinho alijiunga na United mwaka 2016 kwa mkataba wa miaka mitatu uliokuwa unamalizika majira ya kiangazi mwakani, lakini sasa ameongeza mwaka mmoja hadi 2020 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine mmoja.
Manchester United leo itakuwa ugenini kwenye mji wa Yeovil kucheza na timu ya ligi daraja la pili Yeovil Town FC kwenye mchezo wa raundi ya nne ya kombe la FA.
Hakuna maoni: