Breaking

'Subalheri' haitakuwa ya mwisho,

Image result for Subalheri
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Aslay, ameweka wazi sababu ya kufanya kazi na Nandy mara kwa mara na kusema kwamba mashabiki wanawasababisha wafanye hivyo.


Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Aslay amesema mashabiki walifurahishwa baada ya kufanya kazi ya kwanza yeye na Nandy, na ndipo walipoona ni vyema wakarudi tena studio kufanya kazi nyingine kwa ajili yao.

"Ni pendekezo la mashabiki, tumeona mashabiki wakitaka kitu kingine kutoka kwetu baada ya kazi ya kwanza na Nandy,tukaona ni vyema tuingie jikoni kuwapa kitu kingine maalum kwa ajili yao", amesema Aslay.

Pamoja na hayo Aslay amesema kazi hii ya sasa ambayo wameifanya 'Subalheri' haitakuwa ya mwisho, kwani kuna zingine nyingi ambazo wanatarajia kuzifanya kwa pamoja. 

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.