Marekani inaweza kufikiwa na silaha za nyuklia za Korea Kaskazini
Korea Kaskazini Kim Jong-Un amelihutubia Taifa lake January 1, 2018 katika sherehe za mwaka mpyahotuba ambayo imerushwa LIVE na vituo mbalimbali vya television nchi humo.
Kim Jong-Un amesema kuwa ana kitufe cha kubonyeza cha silaha za nyuklia kipo kwenye meza yake wakati wowote anaweza kukitumia, hivyo Marekani isithubutu kuanza vita.
“Marekani inaweza kufikiwa na silaha za nyuklia za Korea Kaskazini, kweli na wala sio vitisho.” – Kim Jong-un
Mbali na hilo, pia Kim ametoa wito kwa Korea Kusini kwamba anawakaribisha kwenye mazungumzo.
Taifa la Korea Kaskazini limewekewa vikwazo zaidi mwaka uliopita 2017 kutokana na mipango yake ya silaha za nyuklia na majaribio ya mara kwa mara ya silaha hizo.
Hakuna maoni: