YANGA YACHOSHWA NA KATIBU WAO
KLABU ya Yanga imeonyesha hali ya kuchoshwa na
tabia ya Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga Ibrahim Akilimali za kupinga
mabadiliko ya klabu hiyo hivyo imewalazimu kutoa mapendekezo ya kumfuta
uanachama.
Mwishoni mwa wiki iliyopita Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alitangaza rasmi nia ya klabu hiyo kuanza mchakato wa kwenda katika mfumo wa hisa jambo ambalo baadae Akilimali alisikika akipinga mfumo huo na kuomba Yanga wamtake radhi.
Akizungumza ndani ya Makao Makuu ya Yanga Makamu Mwenyekiti wa Tawi la Uhuru, Kaisi Edwin alisema, wamekutana wenyeviti wote wa matawi na kukubaliana kuandika barua kwa uongozi huo ili wamfutie uanachama mzee Akilimali.

Hakuna maoni: