Breaking

Aubameyang kesho hatokuwepo kwenye mechi ya Everton


Kupitia kikao chake na waandishi wa habari mapema hii leo meneja wa klabu ya Arsenal, Arsena Wenger ameonekana kuwakatisha tamaa mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kufuatia kusema kuwa huwenda mchezaji wao mpya waliyomsajili kutokea Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang hatokuwemo katika kikosi kitakacho ikabili Everton hapo kesho siku ya Jumamosi.

Wenger amesema kuwa mchezaji huyo anasumbuliwa na ‘virus’ na anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo huku akiongeza kuwa Henrikh Mkhitaryan ataanza katika mechi hiyo.

“Siku hizi ligi ya England inachangamoto kwa kwa kila mchezaji mkubwa,  Aubameyang hupenda staili ya mpira tunaoucheza na naamini anahitaji changamoto mpya,”amesema Wenger.




Arsena Wenger ameongeza “Wachezaji wao hucheza pamoja na kwa sasa wanamaelewano mazuri ni matumaini yangu.”

Aubameyang atakuwa akivaa jezi namba 14 ndani ya Emirates baada ya kukamilisha usajili uliyoweka rekodi ya klabu hiyo wa paundi milioni 56 akitokea Borussia Dortmund.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.