Breaking

Nandy afunguka kuhusu kuimba wimbo wa ruby

Image result for nandy
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye kwa sasa anafanya poa zaidi kwa upande wa wasichana, Nandy, amegoma kabisa kuimba wimbo wa msanii mwenzake Ruby ambaye inaaminiwa hawapikiki chungu kimoja.

Nandy akiwa kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na East Africa Televisio, aliombwa na mtangazaji huyo kuimba wimbo wa Ruby wowote kama kweli anamkubali msanii huyo, kitendo ambacho Ruby alishawahi kukifanya kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na Nandy kugoma kabisa kufanya hivyo.

Alipoambiwa kuimba wimbo wa Ruby, Nandy alidai kwamba sio lazima kwa yeye kufanya hivyo, kwa kuwa Ruby aliimba yakwake, kitu ambacho huenda kikabua minong'ono zaidi juu ya kutoelewana kwa wawili hao.

Pamoja na hayo Nandy amejibu kitendo cha Ruby kusema kuwa yeye aliona ni vuema kumuachia nafasi na yeye asikike, na kusema kwamba sio kweli kwamba alimpisha, kwani alikuwa na kazi zake alizozitoa lakini hazikufanya vizuri kama alivyotegemea.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.