Tutawatangaza Hadharani Wake Zao Wajue Wanawatoto wa Nje ya Ndoa- Makonda
Paul Makonda amefunguka na kusema wanaume ambao wamewazalisha wanawake na kuwatelekeza bila kuwapa matunzo pindi watakapoitwa wakikaidi wito huo kwa lengo la kulinda ndoa zao basi watawatangaza hadharani ili wake zao wajue wana watoto nje ya ndoa.
Makonda amesema hayo leo katika ofisi zake wakati akiongea na mamia ya wanawake ambao wametelekezwa na wanaume zao baada ya kuzalishwa, katika mkutano huo Makonda ametangaza kuwa jambo hilo litakwenda kwa siku tano mfululizo ili kutoa nafasi kwa wanawake wote wenye matatizo hayo kuweza kusikilizwa.
"Kama tukikuita hutaki, unajificha unajidai kulinda ndoa yako wakati mama yangu huku anateseka na mtoto huku sisi tutakuanika hadharani mkeo ajue una mtoto wa nje ya ndoa, mimi najua sijaanza leo kupigana hii vita najua wakina baba wasiopenda matokeo yao watanichukia lakini ukinichukia, ukinitukana, kunifedhehesha ni kama unanipaka mafuta yanayoning'arisha zaidi chuma kinaimarishwa na moto na viongozi wanaimarishwa na kebehi" alisisitiza Paul Makonda
Hakuna maoni: