Breaking

JIBU LA VANESSA KWA JUX


Baada ya taarifa kuwa nyingi Image result for Jux na vanessa Vanessa Mdee na Jux kurudiana, hatimaye Vanessa amejibu ukweli wa suala hilo.
Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Bounce’ amekiambia kipindi cha The Playlist, Times Fm kuwa hawajarudiana bali kilichopo sasa ni urafiki tu.
“Kitu ambacho nyie hamjui Jux ni mshikaji wangu ni mtu ambaye tunapatana na kufanya kazi pamoja hata vitu vingi ambavyo ni nje ya sekta ya muziki Jux anasapoti, hatuwezi kuanza kugombana na sasa hivi, tunakuwa tunaharibu biashara” amesema.
Vanessa na Jux walikuwa wapenzi na kipindi cha mahusiano yao waliweza kutoa wimbo wa pamoja uitwao Juu pamoja na kushirikishwa katika ngoma ya Nikki wa Pili ‘Safari’.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.