Breaking

ATIMAE SERIKALI YAACHIA AJIRA ZA WALIMU

Serikali imetangaza kutoa ajira mpya za walimu wa shule za msingi na sekondari hii leo, ambapo jumla ya walimu 3033 wamechaguliwa na kupangiwa vituo vya kazi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleiman Jafo, akiongea na waandishi wa habari leo, ametangaza kuwa walimu wamechaguliwa ili kwenda kuziba nafasi iliyoachwa wazi na walimu waliobainika kuwa na vyeti feki baada ya zoezi la uhakiki kukamilika.

“Majina ya walimu yanayotangazwa leo yanatokana na tangazo la serikali la kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwa walimu katika shule za msingi na sekondari waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi mapema mwaka huu ambapo mnaklumbuka zoezi hili lilikuwa linafanyika kupitia Ofisi ya Rais utumishi,” amesema Waziri Selemani Jafo.

Waziri Jafo ameeleza kuwa kati ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi walimu 266 ni wa shule za sekondari na walimu 2767 ni wa shule za msingi na kuwataka waripoti ndani ya muda uliowekwa ambao ni kuanzia Disemba 27, 207 mpaka Januari 7, 2018 wakiwa na vyeti halisi vya elimu pamoja na cheti cha kuzaliwa.

“Baada ya uhakiki wa maombi ya walimu yaliyotumwa serikalini, jumla ya walimu 3033 wamechaguliwa kupangiwa viyo vya kazi. Kati yao walimu 266 ni wa sekondari na 2767 ni wa shule za msingi. Walimu hao wanatakiwa kuripoti katika Walimu hao wanatakiwa kuripoti kuanzia tarehe 27 Disemba 2017 hadi Januari 7, 2018 wakiwa na mahitaji yafuatayo. Wawe na vyeti halisi vya taaluma ya kidato cha tano na cha sita, awe na cheti cha kitaaluima cha kuhitimu mafunzo ya ualimu kwa ngazi husika na mwish awe na cheti cha kuzaliwa,” amesema Jafo.

Aidha amewatahadharisha waajiriwa wapya kuhakikisha kuwa wanaripoti katika vituo walivyopangiwa kwa wakati na kuwaonya kutohama vituo vyao vya kazi pasipo kupata ridhaa kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Waajiriwa wapya wanatahadharishwa kuriporti katika shule husika na hatutarajii mtu mmoja kuhama kutoka shule moja na kwenda nyingine ndani ya halmashauri au mkoa wake bila ridhaa ya Ofisi ya Rais TAMISEMI,” alionya Waziri Jafo.

Hakuna maoni:

Inaendeshwa na Blogger.